Header

Vanessa Mdee ajibebea dili nono la Universal Music Group

Staa wa Bongo Fleva, Mwimbaji kutoka Mdee Music, Vanessa Mdee amepanda kwenye kiwango cha kimataifa zaidi kwa kuingia katika mkataba wa kibiashara na kampuni ya Universal Music Group(UMG).

Kupitia ukurasa wake wa Instgram, Vanessa ameweka ujumbe wa kutoa shukrani za dhati juu ya hatua hiyo kuelekea kwa mashabiki waliohusika kwa namna yoyote mpaka afike alipo kwa sasa kisha akatoa habari njema ya kuwa ni kwa mara ya kwanza kwa msanii wa Kiafrika kupata dili hilo alilothibisha kuwa ni dili lenye mkwanja mrefu sana.

Vanessa alipost.

“Kama ilivyo ada, tunaanza kwa kumshukuru mwenyezi mungu kwa baraka zake na kibali chake cha kutufikisha siku njema ya leo.

Nawashukuru mashabiki wangu, ndg, jamaa na marafiki wa karibu, tuliokuwa sambamba tangu mwaka unaanza mpaka hivi sasa tukielekea ukingoni.

Nimeona niitumie siku na fursa hii kuwajulisha wapendwa mashabiki zangu;
Mwanzoni mwa mwaka huu,
Nilipitia changamoto nyingi Sana
Lakini kwa neema za Mungu , Nilitoka mahali pale na sio kuona baraka tu bali na maajabu mengi yaliyotokea kwenye maisha yangu .
Ikiwemo kuwa mmoja wa familia ya Universal Music Group in a unique joint signing between @universalmusicgermany@airforce1 na @universalmusicgroup na hii ni mara ya kwanza kwa Msani wa Kiafrika kupata deal ya aina hii yenye mkwanja mrefuuuuuuuuuuu sana 🙌🏽. Hii ni habari njema kwa mashabiki wangu na ndiyo kwanza tumeanza. Mambo makubwa zaidi yanakuja 🙏🏾. Kumbuka kila mwisho wa Jumapili ndiyo mwanzo wa Jumatatu, usiogope kuanza upya.”

Kama ilivyo ada, tunaanza kwa kumshukuru mwenyezi mungu kwa baraka zake na kibali chake cha kutufikisha siku njema ya leo. Nawashukuru mashabiki wangu, ndg, jamaa na marafiki wa karibu, tuliokuwa sambamba tangu mwaka unaanza mpaka hivi sasa tukielekea ukingoni. Nimeona niitumie siku na fursa hii kuwajulisha wapendwa mashabiki zangu; Mwanzoni mwa mwaka huu, Nilipitia changamoto nyingi Sana Lakini kwa neema za Mungu , Nilitoka mahali pale na sio kuona baraka tu bali na maajabu mengi yaliyotokea kwenye maisha yangu . Ikiwemo kuwa mmoja wa familia ya Universal Music Group in a unique joint signing between @universalmusicgermany @airforce1 na @universalmusicgroup na hii ni mara ya kwanza kwa Msani wa Kiafrika kupata deal ya aina hii yenye mkwanja mrefuuuuuuuuuuu sana 🙌🏽. Hii ni habari njema kwa mashabiki wangu na ndiyo kwanza tumeanza. Mambo makubwa zaidi yanakuja 🙏🏾. Kumbuka kila mwisho wa Jumapili ndiyo mwanzo wa Jumatatu, usiogope kuanza upya. @mdeemusicofficial #SwimmingInJesusJuice #MoneyMondays #MoneyMondaysTheAlbum #SheKing #HistoryInTheMaking #Tanzania #CultureCustodian #VanessaMdee #Pioneer #AndAllGodsPeopleSaidAmen #AfricaToTheWorld #BlackGirlMagic

A post shared by VeeMoney (@vanessamdee) on

Hata hivyo Vanessa ni msanii anayetajwa kuipeperusha kwa ustadi na nguvu zote bendera ya Tanzania kupitia muziki ambaye pia kwa mwaka huu wa 2017 ameingia kati ya wasanii walipata kushrikishwa kwenye album ya kimataifa ya Diamond Platnumz ‘A Boy From Tandale’ inayotarajiwa kununulika sokoni kuanzia tarehe 12 Januari, 2018.

Comments

comments

You may also like ...