Header

Y Tony afunga na mchanganyiko wa ‘Charanga’ na ‘Bongo Fleva’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Heri Michael ‘Y Tony’ ameachia rasmi kazi yake mpya chini ya uandaaji wa mikono ya maprodyuza wawili ‘Zest Pro’ na Mr. LG kutoka Studio za Moja Moja Records.

Chini ya lebo hiyo ambayo pia ni kiwanda cha kuandaa kazi za sanaa(Music/Audio) inayobaki kwa utambulisho wa jina la Moja Moja Records, Y Tony ameamua kufunga mwaka kwa ngoma inayokwenda kwa jina ‘Tukajichane’ ikiwa imetoka sambamba na video yake, Video iliyoandaliwa na kuongozwa kwa usimamizi Director Travellah/Msafiri wa Kwetu Studios.

Hata hivyo Staa huyo wa ngoma ya ‘Masebene’ kwa mwaka wa 2017 inahesabiwa kuwa ameachia nyimbo kadhaa zilizofanya vizuri kama vile ‘Kivuli’ na ‘Kibenten’.

Comments

comments

You may also like ...