Header

Jezi namba 8 na 24 za Kobe Bryant ‘zastaafishwa’ rasmi

Jezi namba 8 na 24 za Mchezaji wa zamani wa Timu ya Kikapu ya Los Angeles Lakers Kobe Bryant zimestaafishwa rasmi na Klabu hiyo siku ya Jumanne asubuhi wakati wa Mchezo wa Lakers Dhidi ya Golden State Warriors uliopigwa katika Dimba la Staple Center.

Tukio hilo liifanyika wakati wa Mapumziko kwenye Mchezo ambao Warriors walishinda kwa jumla ya alama 116 dhidi ya 114 za Lakers.

Gwiji huyo ambaye amecheza Miaka yote 20 katika Timu hiyo anakuwa Mchezaji wa kwanza katika historia ya Mchezo wa kikapu ambaye jezi zake mbili zimestaafishwa.

Katika Miaka 20 aliyochezea Lakers Kobe Bryant alitumia jezi namba 8 katika Kipindi cha Miaka 10 ya Mwanzo akishinda ubingwa mara tatu mfululizo wa NBA. Alibadili jezi Mwaka 2006 na kutumia namba 24 ambapo alishinda makombe mawili mengine ya NBA na kufanikiwa kufikisha Mataji 5 mpaka anastaafu Mwaka 2016 akiwa na miaka 38.

Comments

comments

You may also like ...