Header

Vita ya Salah, Mane na Aubameyang hatma yake kujulikana Januari 2018

Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF limetoa orodha ya mwisho ya Wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji bora wa kiume wanaocheza nje ya Afrika. Majina ya Wachezaji hao ni Sadio Mane, Mohamed Salah pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang.

Sadio Mane na Mohamed Salah wanacheza katika Klabu ya Liverpool inayoshiriki Ligi kuu nchini England huku Salah akiwa ndiye kinara wa Magoli katika Klabu ya Liverpool Msimu huu huku pia akiwa ndiye kinara wa Magoli katika Ligi hiyo akiwa na jumla ya Magoli 19 huku pia akiisaidia timu yake ya Taifa ya Misri kufuzu kombe la Dunia tangu Mwaka 1990. Mane amekuwa na Msimu mzuri pia katika Klabu ya Liverpool pamoja na Timu yake ya Taifa ya Tunisia akiisaidia kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu Mwaka

Aubameyang ambaye alishinda Tuzo hiyo Mwaka 2015 licha ya kutokuwa na Msimu mzuri kwa Klabu yake ya Borrusia Dortmund mpaka sasa amefunga Magoli 13 katika Michezo 15 ya mwisho.

Mshindi wa Tuzo hiyo atajulikana Januari 4 Mwkani mjini Acrra nchini Ghana, Je atakua Mohamed Salah ambaye ametoka kushinda tuzo ya kituo cha BBC ya mchezaji bora au atakua Sadio Mane au Aubameyang atanyakua mara ya pili majibu yatafahamika Januari Mwakani.

 

 

Comments

comments

You may also like ...