Header

Arsenal na Man City zatinga nusu Fainali Carabao Cup

Usiku wa Jana Mashindano ya Kombe la EFL Cup maarufu Kama Carabao Cup yaliendela kwa Michezo miwili ya Robo fainali kupigwa. Arsenal na Man City zikikata tiketi za kutinga nusu Fainali.

Leicester City ambao ni Mabingwa wa Ligi kuu nchini England Msimu wa 2015-2016 waliwakaribisha Manchester City katika Dimba la King Power Stadium Mchezo ambao vijana wa Pep Guadiola walishinda kwa Penati 4-3 baada ya kutoka sare ya 1-1 kwa Dakika 90 pamoja na zile za nyongeza. Magoli yalifungwa na Bernado Silva dakika 26′ huku Vardy akisawazisha dakika dakika ya 96 ya Mchezo baada ya dakika 7 kuongezwa.

Arsenal walikuwa katika Uwanja wao wa nyumbani wa Emirates wakiwakaribisha West Ham United Mchezo ambao Arsenal walishinda kwa Goli 1-0 Welbeck akifunga goli hilo pekee dakika ya 42′ na kukata tiketi ya kutinga nusu Fainali ya Michuano hiyo.

Michezo miwili iliyobaki itaendelea tena hii leo, Mabingwa watetezi wa Kombe hilo Manchester United watakuwa wageni wa Klabu ya Bristol City huku Mabingwa wa England Klabu ya Chelsea wakiwa nyumbani kuwakaribisha Bournemouth.

Comments

comments

You may also like ...