Header

BAADA YA DOGO RICHIE KUONEKANA KWENYE STUDIO ZA PACHO ENTERTAINMENT MATOKEA NI IJUMAA HII!

Dogo Richie Kushoto Akiwa Na Mdau wa Muziki Ndani Ya Studio Za Pacho

Msanii kotoka Kenya maarufu kama Dogo Richie, amekuwa akiwaacha wengi midomo wazi kwa jinsi mwaka huu alivyobadilisha mtindindo wake wa kutoa vibao vya muziki. Mkali huyo wa muziki majanga kwasasa ameamua kuwapa mashabiki wake ladha tamutamu za muziki kupitiliza kwani mwezi mmoja tu baada ya kuachia kibao chake kipya kwajina Ngojea sasa ametimba kwenye studio za Pacho Entertainment na tayari ametoa jina la kibao chake kijacho kwajina SAWA.  Studio za Pacho zilizoko mji mkuu wa Kenya Nairobi zinamilikiwa na mwanamuziki Rapdamu na ni maarufu kwani zilichangia kumtoa mwanamuziki Timmy Tdat kupitia kibao chake Wele wele. Pia vibao kama Tunakubali yake Timmy Tdat x The Kensoul. Usisahau pia King kaka pamoja na msanii Rich Movoko kabla ya kuhamia wasafi walitoa kibao ”Lini”.

Dogo Richie Kulia Akiwa Na Mdau Wamuziki Ndani Ya Studia za Pacho.

Hata hivyo kuna vibao vingi ambavyo vimetoka kupitia studio hii, na mara hii ni zamu ya SAWA kibao kutoka kwa staa Dogo Richie ambaye amesema kitatoka Ijumaa hii. Akiongea na meza yetu ya habari ya Dizzim News, Richie amesema ameamua kufata mkondo wa wasanii kama  Diamond Platnumz anavyofanya. Maana muziki ni biashara na msanii akitaka kufaulu nilazima ajitume zaidi ya kawaida ndio aweze kufikia malengo. Mpka sasa Richie anakadiriwa kufanikiwa kuwafunika wasanii wenzake ambao wanafanya muziki katika Pwani ya Kenya. Huku akiongoza jedwali kama msanii wa Pwani ya Kenya aliyezoa Show nyingi za muziki mwaka wa 2017. Hata hivyo Richie ameanza mikakati ya kupania kuchukua nafasi za juu kwenye muziki wa kizazi kipya Africa Mashariki na Africa kwa ujumla, kwani anasema uwezo ako nao.

 

Comments

comments

You may also like ...