Header

MFAHAMU VICMASS LUODOLLAR RAPPER WA NCHINI KENYA ALIYEPITIA MENGI KABLA KUFAULU KIMAISHA!

Vicmass Luodollar

 

Katika muziki wa kufoka Africa Mashariki, umekua na changamoto nyingi ila wasanii wakufoka maarufu kama rappers hawajafa moyo na kila uchao wanazidi kuchipuka. Kutoka Kenya wengi wanamfahamu rapper wa kimataifa maarufu kama Octopizzo. Octopizzo nikati ya mastaa ambao historia zao za maisha ni zakutia moyo kwaani walianzia  chini lakini kwasasa wanamiliki mali zenye thamani ya juu. Sasa basi kupitia Octopizzo kuna msanii ambaye kwasasa anawakilisha vyema muziki wa kufoka hapa nchini Kenya ambaye naye maisha yake ni sehemu moja ya kutia moyo hasa kwa wasanii wachanga ambao wanaota kuja kuwa mastaa wakubwa mbeleni. Vicmass Luodallar ni jina lakupigiwa mstari, kwasasa unapomtaza kwenye runinga ama kumusikiliza kwenye radio, unaweza dhania ni mtoto wa bwenyenye mkubwa ama alilelewa kwenye familia ya kitajiri ila la.

Mzazi Tuva, Shaz na Vicmas Luodollar

Vicmass katika maisha yake yote amekuwa mtu wa kuhaha, ”Babangu alifariki dunia nikiwa na miaka mitano pekee, kwahivyo sikuwahi kumfahamu zaidi. Na baada ya hapo maisha yaligeuka kuwa uchungu, maana hata shule niliacha katika hatua za mwanzo kabisa kisa na maana kutafutia familia yangu yaani mama na ndugu zangu wadogo wawili.” Vicmass alimwambia mtangazaji wa radio Citizen ya nchini Kenya Mzazi Willy M Tuva. Vicmass ameshawahi kutafuta kazi sehemu mbambali za nchini Kenya na hata kwamaranyingine alijikuta mjini Emali kati jimbo la Makueni akifanya kazi ya machinga.

Vicmas Luodollar akiwa katika harakati zake za kuchapa kazi ya umachinga mjini Emali

”Nilishafanya kazi ya machinga pale Emali, ilinibidi nijitume kwa mda wa ziada ili nitengeneze pesa zaidi, pesa ambazo nyingine nilizituma nyumbani kwa mama na nyengine nilitumia kuingia studio ili kurekodi muziki.” Alizidi kufunguka Msanii Luodollar. Vicmass kwasasa anaishi maisha bora kupitia muziki wake, huku kibao chake kilichomtambulisha Bank Otuch kikizidi kufanya vizuri kwenye radio tofauti nchini Kenya. Akiongea na Radio Citizen, Luodollar amesema ana kazi alizomshirikisha Juma Nature kutoka Bongo na wasanii wengine malejendari wa hapa Kenya na Africa Mashariki huku pia ameanza kufikiria kuwashirikisha wasanii chipukizi na tayari jana alimutambulisha mtoto mkali wa kike kwa jina Shaz kupitia kazi yao ya pomoja kwajina nishike. Itazame video ya wimbo huu ”Nishike” hapa chini kwenye channel YouTube.

Comments

comments

You may also like ...