Header

Khloe Kardashian na Tristan wathibitisha matarajio ya mtoto

Kutoka kwenye familia ya Kadashians, mfanyabishara mjasiriamali na mwanamitindo kutoka Marekani, Khloe Kardashian hatimaye ameweka hadharani habari ya kuwa anategemea kupata mtoto kwakuwa ni mjamzito.

Khloe aliweka kumbukumbu ya picha ya tumbo lake mtandaoni akiwa ameshikiwa tumbo hilo kwa mikono miwili na mpenzi wake Tristan Thompson. Katika picha hiyo aliandika, “Najua tumekuwa kimya lakini tulitaka tufurahie hiki kati yetu, familia na marafiki wa karibu kwa muda mrefu tulilifanya hili faragha”.

Hata hivyo, uvumi na habari za wapenzi hao wawili kutarajia mtoto zilianza kuingia kwenye masikio ya baadhi ya fatiliaji mwezi Septemba.

Comments

comments

You may also like ...