Header

Diamond Platnumz agusia tena ukali wa ujio wa kazi ya Marombosso chini ya WCB Wasafi

STAA wa Bongo Fleva na hitmaker wa ngoma ya WAKA aliyomshrikisha rapa Rick Ross, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz, amegusia kwa mara nyingine ujio wa kazi ya msanii Marombosso na kuonesha shahuku ya kazi hiyo kuwafikia mashabiki kulingana na uzuri wake.

Marombosso ambaye imeshathibitika kuwa atakuwa akifanya kazi chini ya lebo ya WCB Wasafi kwa mujibu wa viashiria tofauti, Diamond Platnumz amepost picha kupitia ukursa wake wa Instagram akiwa na Marombosso na kuandika ujumbe wa kuwa “Nimejaribu kusubiri ulimwenguni usikie kile ulicho nacho kwa ajili yao  na kumtag Marobosso ‘@mbosso_’ kisha kumaliza na alama ya Reli yenye kitambulishi cha neno #TheAfricanVoice.

BLACK BOTTLE BOYS!!! @mbosso_

A post shared by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Marobosso naye kupitia ukurasa wake wa Instagram alionesha kuwa kuna kitu kiko tayari na kikubwa ni muda tu kwakuwa katika picha aliyoweka akiwa na Diamond Platnumz alikutwa na maneno yanayozungumza kuwa muda utazungumza ‘PRAY HARD & FIGHT HARD ..”Time will surely tell” na kumtag Diamond Platnumz ‘@diamondplatnumz’.

PRAY HARD & FIGHT HARD .."Time will surely tell" @diamondplatnumz

A post shared by The African Voice 🌍 (@mbosso_) on

Hata hivyo Marombosso tayari ameashaanza kutumia neno hilo la ‘TheAfricanVoice’ kama moja ya kitambulishi chake katika kuweka msisitizo wa jna lake hasa katika ukanda huu wake wa biashara ya muziki akiwa ni msanii wa kuimba mwenye sifa ya uandishi na Sauti.

 

Comments

comments

You may also like ...