Header

Swizz Beatz ayapanda mabega ya mkewe Alicia Keys mbele ya watoto

Mtayarishaji wa muziki kutoka Nchini Marekani, Swizz Beatz amesherehekea siku kuu ya Christmass kwa picha ambayo imemuonesha hali ya haki sawa kwa pozi la mikono juu akiwa ni mwenye kubebelea chupa mbili za vinywaji huku akiwa kabebwa mabegani na mkewe Alicia Keys.

Picha ya Swizz akiwa na familia yake kwa kuzungukwa na wanae iliyoonekana kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instgram, imeleta picha nyingine ya tofauti kuwa upo uwezekano wa mwanamke kufanya kile kilichohisiwa kufanywa na Mwanaume na picha hiyo imeongeza mjadala wa kusifia kwa mbali kwa kuitaja caouple hiyo bila shaka inaweza kutafsiriwa kuwa ni yenye furaha na upendo wa haina yake kati yao na familia kwa ujumla.

Hata hivyo kingine kinachotazamiwa ni siku moja baada ya Boxing Day yaani tarehe 27 Mwezi huu wa Disemba Swizz Beatz atakuwa na siku ndefu ya kuikumbuka siku na tarehe ya kuzaliwa kwa mwanae wa kiume, Genesis Ali Dean ambaye atakuwa anatimiza umri wa miaka mitatu.

Comments

comments

You may also like ...