Header

Fid Q na Prodyuza Luffa waingia chimbo walikokutana na Saida Karoli

Rapa na muandishi kutoka Tanzania, Fareed Kubanda a.k.a Fid Q ameingia studio za Wanene na kuandaa kikubwa ambacho amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kwakuwa ni kikubwa na cha kuishangaza dunia kutokana na hisia, uwezo na ushirikiano uliweka katika kukiandaa.

Shahuku ya Fid Q ilidhihirika wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa picha aliyoipost akiwa studio na mtayarishaji Luffa huku kwa mbali akionekana mtu aliyeonekana kuwa kama ni Joh Makini kwa mbali na pembeni akionekana rapa Motra The Future kutoka Arusha.

Fid Q aliweka maelezo katika picha hiyo, “I can’t wait for the whole world to hear this… S/O to @kingluffa for holding everything down like gravity…!!!”

Luffa ambaye anaonekana kuwa ni muandaaji wa kinachofanyika, naye siku chache kabla aliweka picha hiyo bila kuweka maelezo marefu na kuweka kutambulishi cha alama ya reli ya ##vlone.

#vlone

A post shared by luffa @wanenestudios (@kingluffa) on

Hata hivyo kabla prodyuza Lufa wiki iliyopita alishaweka picha yake akiwa na Fid Q na mwimbaji mkongwe Saida Karoli na kuthibitisha kuwa wameandaa kazi ya pamoja.

“Studio session with @therealfidq & @saidakarolitz” Aliandika Luffa.

Studio session with @therealfidq & @saidakarolitz #wecooking

A post shared by luffa @wanenestudios (@kingluffa) on

Comments

comments

You may also like ...