Header

Idris Sultan afunga na hii kwa mwaka 2017

Muigizaji na kijana mwenye ushawishi kutoka Tanzania, Idris Sultan amefunga kuweka jumbe na picha katika ukurasa wake wa Instagram na kutoa shukrani za kutosha kwa kila aliyeshiriki na namna yoyote ya kufika alipo sasa hata kuutaja mwaka 2016 kuwa ni mwaka ambao alifikia kiasi kidogo cha mafanikio tofauti na 2017.

Kikubwa mbali na kuwashukuru mashabiki, mashabiki na wazazi wake, Bi. Naima na baba yake Bw. Rashid, Idris amesema kuwa picha na ujumbe huo alioweka katika ukurasa wake wa Instagram ni post yake ya mwisho kwa mwaka 2017 na kuwahaidi kuwa mwaka 2018 utakuwa ni mwaka wa kufanya makubwa kwa mujibu wa maneno yake.

Idris alipost picha na kuweka kuweka ujumbe huu “Naomba niwashukuru sana kwa mengi tuliyopitia wote 2017 na makubwa mengi tuliyofanya. 2016 haukua mwaka mkubwa sana kwangu ila 2017 wote tumeona mangapi tumefanya na naomba niseme haya sijayafanya mimi tu ila pongezi kubwa sana to my team ikiongozwa na @docta_ulimwengu , kuna sehemu najiuliza nimepitaje ila nakumbuka kuwa kila siku nina dua za Mama yangu Naima na baba yangu Rashid naomba Allah awape nguvu na mkumbuke hata nyinyi ndoto zenu mnaweza kuzifuata hata sasa, ndugu zangu wote wa CMG, media zote pamoja na blogs na ningependa kusema nina the most amazing fans. Sultans mna nguvu bila kelele na nawapenda na kuwakubali sana Tunzo zote mwaka huu tumebeba because of you. Nawaahidi 2018 tunawapa hasira zaidi. Hii ni post yangu ya mwisho 2017, sina mda wa kusema new year new man ni upuuzi, nasema new year same man just a better me #iRefuseToStop .. Tukutane 2018 😉 #AllahBlessYou”.

Naomba niwashukuru sana kwa mengi tuliyopitia wote 2017 na makubwa mengi tuliyofanya. 2016 haukua mwaka mkubwa sana kwangu ila 2017 wote tumeona mangapi tumefanya na naomba niseme haya sijayafanya mimi tu ila pongezi kubwa sana to my team ikiongozwa na @docta_ulimwengu , kuna sehemu najiuliza nimepitaje ila nakumbuka kuwa kila siku nina dua za Mama yangu Naima na baba yangu Rashid naomba Allah awape nguvu na mkumbuke hata nyinyi ndoto zenu mnaweza kuzifuata hata sasa, ndugu zangu wote wa CMG, media zote pamoja na blogs na ningependa kusema nina the most amazing fans. Sultans mna nguvu bila kelele na nawapenda na kuwakubali sana Tunzo zote mwaka huu tumebeba because of you. Nawaahidi 2018 tunawapa hasira zaidi. Hii ni post yangu ya mwisho 2017, sina mda wa kusema new year new man ni upuuzi, nasema new year same man just a better me #iRefuseToStop .. Tukutane 2018 😉 #AllahBlessYou

A post shared by Idris Sultan 🇹🇿 (@idrissultan) on

Idris Sultan anetegemewa kuonekana katika kazi kadhaa kubwa zake na baadhi za kushirikishwa kwa kuwa ni mipango mingi imebainika mwaka huu wa 2017 kuwa atashiriki kibiashara na wadau wakubwa wa filamu, na katika hilo la Idris inaweza akasogea zaidi kwenye hatua ya ndoto zake za kufanya kazi katika viwango vikubwa vya kimataifa ‘Hollywood’.

Comments

comments

You may also like ...