Header

Vanessa Mdee na Mimi Mars washirikiana na Ndugu yao kwenye wimbo Mpya ‘Beautiful JESUS’

Waimbaji wa muziki wa Bongo fleva Tanzania kutoka katika familia ya Mzee Sammy Mdee, Mimi Mars na Vanessa Mdee wameonekana katika ushirikiano wa wimbo mpya wa ndugu yao  Nancy Namtero Tero Mdee ‘Nancy Hebron’ unaokwenda kwa jina’Beautiful JESUS’.

Awali kilisambaa kipande kilichonesha Vanessa Mdee na Mimi Mars wakionekana kuwa location na Nancy yakabaki maswali ya kutaka kujua nini kianaadaliwa na hatimaye Mimi Mars na Vanessa Mdee wamesikika watika beti tofauti nao wakiimba juu ya uzuri wa Yesu kulingana na wazo la wimbo huo mpya.

Kuonesha umoja wao ulilenga kutuma ujumbe wa wimbo huo, Wote kwa pamoja wamejistili kwa mavazi marefu kitu ambacho kimeipamba kwa uzuri kabisa video ya wimbo huo.

Hata hivyo Nancy kwa mwezi huu wa Disemba ameachia nyimbo tatu sambamba na video zake ambazo ni Malaika, Hakuna cha Kunitoa kwa Yesu na hii mpya ‘Beautiful Jesus’.

Itazame Video ya Malaika.

Itazame video ya wimbo ‘Hakuna Cha kunitoa kwa Yesu.

Comments

comments

You may also like ...