Header

Birdman matatani kwa kushindwa kulipia mkopo wa mjengo wake

Bosi wa Cash Money Records, Birdman yupo matatani. Anakabiliwa na deni la dola milioni 12 kwa kushindwa kulipia deni la nyumba.

Na sasa moja kati ya nyumba zake, ikiwemo yenye futi za mraba 19,970 ya Miami Beach na ile yenye futi za mraba 26,040 ya North Miami ambayo ndani ina studio za kurekodi muziki ya Hit Factory Criteria zinaweza kushikiliwa.

Mkopo huo alipewa na kampuni ya Chemtov Mortgage Group Corp.

Bosi huyo amekuwa akitaka kuiuza nyumba yake aliyoinunua mwaka 2012 kwa dola milioni 14. Aliiweka sokoni mara ya kwanza dola milioni 20 na sasa bei imeshuka hadi dola milioni 16.9.

Comments

comments

You may also like ...