Header

Don Jazzy ajitosa kumpata Rihanna

STAA wa muziki kutoka nchini Nigeria na muanzilishi wa lebo ya muziki ya Mavin Records, Michael Collins Ajereh ‘Don Jazzy’ amejitosa mzima mzima kumsaka mrembo na Mwimbaji mzaliwa wa Barbados, Robyn Rihanna Fenty ‘Rihanna’.

Picha iliyosambaa kwa kasi ndani ya muda mfupi iliyomuonesha Rihanna akiwa ni mwenye kujiachia kwa mkao wa kuvutia kwenye kiti ndani ya gauni jepesi la rangi nyekundu, Don aliiweka picha hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika ujumbe wa kuwa yuko nchini Barbados na anahitaji kujua Rihanna yuko meneo gani ya nchi hiyo.

“Baby boo I’m in Barbados too where re you? 😘😘” Don Jazz Aliandika.

Baby boo I’m in Barbados too where re you? 😘😘

A post shared by DON JAZZY 🇳🇬 (@donjazzy) on

Hakika Post hiyo ya Don Jazz iliyomlenga Rihanna, moja kwa moja ilitafsiriwa na wengi kuwa picha hiyo ya Rihanna inaweza kuwa umemtoa udenda Don Jazzy kwakuwa  inavutia sana katika mtazamo wenye kuzingatia urembo wa Rihanna.

Comments

comments

You may also like ...