Header

Usajili wa Simba Sc hauna tofauti na ule wa Liverpool

Kila Klabu hufanya usajili kulingana na hitaji lake katika eneo husika hususani baada ya dirisha kubwa na Dogo la usajili kufunguliwa, Klabu mbalimbali hutuma ofa zao kwa Klabu zenye dhamana na Wachezaji hao pasipo kuzuiliwa ni Klabu gani suala kubwa sana huwa pesa pamoja na maelewano na taratibu za usajili.

Katika Ligi kuu Tanzania Bara Msimu huu miongoni mwa Vilabu vilivyofanya usajili wa pesa nyingi na kusajili Wachezaji wenye majina Makubwa ni Klabu ya Soka ya wekundu wa Msimbazi Simba Sc. iliamua kuvunja kibubu kwa kusajili nyota zaidi ya 9 kutoka Vilabu mbalimbali wakiweo Haruna Niyinzima kutoka Yanga, John Bocco kutoka Azam na nyota wengine. Licha ya kutumia pesa nyingi Simba imekuwa na kawaida ya kununua sana Wachezaji Vijana, orodha ya Wachezaji kama Shiza Ramadhan kichuya, Mzamiru Yassin, Said Mohamed Nduda, Ally Shomari na Salim Mbonde, Mohamed Ibrahim Mo ni Wachezaji wa Simba ambao wamejiunga na Klabu hiyo wakitokea Mtibwa Sugar.

Simba imekua na kawaida ya kusajili Wachezaji kutoka Mtibwa ndani ya Misimu miwili Simba imesajili si chini ya Wachezjai watano kutoka Klabu moja, ni kama imekuwa sasa Mtibwa ni chuo cha kulelea vijana wa Simba Sc.

Tukielekea kule nchini England tabia ya Simba haina tofauti na tabia ya Majogoo wa jiji Klabu ya Liverpool ambao wamekuwa wakisajili wachezaji wengi kutoka Klabu ya Southampton. Kabla ya kukutajia orodha siku ya Jana Klabu hiyo imekamilisha usajili wa beki wa Kati Virgil van Dijk ambaye ameweka rekodi ya dunia ya kuwa beki ghali Duniani akisajiliwa kwa kititta cha paundi Milioni 75. Beki huyu anakuwa Mchezaji wa nane kusajiliwa na Liverpool akitokea Southampton nyota wengine ni Sadio Mane, Adam Lalana, Peter Crouch, Farnk Lamberty, Nathael Clyne Pamoja na Dejan Lovlen.

 

Comments

comments

You may also like ...