Header

Rayvanny apokea kwa mikono miwili Baraka za mkongwe ‘Hussein Jumbe’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania,Raymond Shaban Mwakyusa ‘Rayvanny’ ameachia wimbo mwingine mpya unaokwenda kwa jina la ‘SIRI’ uliomshirikisha rapa Nikki Wa Pili  chini ya utayarishaji wa Laizer Classic wa Studio za WCB Wasafi, wimbo ambao katika kiitikio kwa asilimia kadhaa umebeba maudhui ya wimbo kwa jina ‘Mapenzi Ya Siri’ wa kipindi cha nyuma wa mwanamuziki nguli wa muziki wa Dansi Tanzania, Hussein Suleiman Jumbe ‘Husein Jumbe’.

Rayvanny ambaye kwa sasa mawazo ya wengi yanatambua kuwa alikuwa aliishia kuingia katika mgogoro wa kutoelewana kimahusiano ya mama wa mtoto wake Faymah, amewaacha watazamaji wa video ya wimbo huo midomo wazi, video iliyoongozwa na Director Eris Mzava kwa kumtumia Faymah kama Video Queen huku  ikabaki bila kubainika kwa haraka kama ilifanyika kabla ya wawili hao kukosane au ni siri yao kwa kinachoendelea.

Imeaminika kuwa nguli wa muziki wa Dansi na muimbaji wa wimbo halisi wa ‘Mapenzi Ya Siri’, Hussein Jumbe ametoa baraka za kutosha juu ya kutumika kwa sehemu ya wazo la wimbo wake kwakuwa ametokea katika kipande cha mwisho cha video ya wimbo huo mpya.

Comments

comments

You may also like ...