Header

Rayvanny na Faymah wafichua siri ya Penzi lao

Msanii wa muziki wa kizazi  kipya kutoka Tanzania, Raymond Shaban Mwakyusa ‘Rayvanny’ na mpenzi wake Faymah wamemaliza tofauti zao baada ya ujio wa ngoma yake ‘SIRI’ iliyomshirikisha Rapa Nikk Wa Pili kutoka WEUSI Kampuni.

Ngoma hiyo amvayo katika Video Faymah ameshiriki kama video Queen imeonekana kuwaunganisha ambapo Rayvanny lupitia ukurasa wake wa instagram aliweka picha waliyopiga kwa pamoja wakiwa location kipindi ambacho video ya wimbo huo ilikuwa ikishootiwa na kuandika ujumbe wa kuwa wawili hao wamerudiana tena.

“Sikukupata kwa Bahati Mbaya Kwanini Nikuache kwa Makusudi NAKUPENDA MAMA JAY ❤❤❤ #SIRI link in My Bio @fahyvanny Embu mtag nawewe roho yako hapa 😂😂 ” Ameandika Rayvanny.

Hata hivyo Faymah kuonesha kuwa wako poa sasa naye aliweka picha ya Rayvanny kutoka katika video ya wimbo huo mpya na kuandika maneno haya ‘Uvumilivu, kusamehe Na Upendo wa dhati Ni Nguzo Ya Wapendanao NAKUPENDA BABA JAY @rayvanny’ Maneno yanayowahakikishia wengi kuwa pendo la wawili hao limerudi kuwa hai.

Itazame video ya wimbo mpya wa Rayvanny ft. Nikki wa Pili – SIRI.

Comments

comments

You may also like ...