Header

Shetta atoa wosia mzito wa kujilinda kwa mwanae ‘Qayllah’

STAA wa muziki wa Bongo Fleva na hitmaker wa ngoma ‘Vumba’ iliyomshirikisha G Nako, Nurdin Bilal Ali a.k.a Shetta amemimina maneno yenye wosia kwa mwanae wa kike, Qayllah Nurdin Bilal kujichunga na wanaume walaghai wenye nia ya kuamuharibia maisha katika siku za usoni.

Shetta anayezidisha mapenzi kwa mwanae huyo, alizma kwenye ukurasa wake wa Instagram na kushusha maneno hayo yenye wosia mkubwa kwa kuandika “Mwanangu Najua kuna watu wanakusubiri subiri ukue kue walete mambo yao ya Kukunyapia nyapia Sasa ninachokuhusia mwanangu Baba Yako nina kila kitu asijudanganye Mtu ukaingia laini ukakazika kijinga jinga Kaza mwanangu…. !! @officialqayllah 👸💪🏾” Shetta alimalizia.

Hii ndo post ya Shetta.

Hata hivyo hofu hiyo imemuingia Shetta kuelekea urembo unaoanza kuchipuka kwa mwanae huyo kwani yapo matukio yenye sura za namna hiyo ambayo utokea kwa watoto katika mazingira ya baadhi ya matukio kuletelezwa kutokana na wazazi kutokewa na ulezi  wa mapema kwa watoto wao na alichosema kinaweza kuwa funzo pia kwa wote wenye watoto kuwa makini na kutatua njia sahihi na kuwafahamisha watoto ili kuliepuka hilo.

Comments

comments

You may also like ...