Header

Wolper Atangaza rasmi kumpiga chini Brown

Mrembo mjasiriamali kutoka Tanzania, Jacqueline Wolper ameondoa utata ulokuwepo juu yake na kijana mjenga misuli na mwanamitindo kutoka Tanzania anayejulikana kwa jina maarufu la Brown.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wolper ametoa taarifa za kuwa ameingia katika penzi zito na mtu ambaye hayuko katika mitandao na utaratibu wa kutembelea kwa wazazi na hatua za ndoa.

Nashukuru sana Mungu kwa kuniamini na kwa kuwa na mm na kuamua kutaka kubadilisha historia ya maisha yangu,ww ni mwanaume ambae umejitoa ili tu niwe wako,umetaka tufike mbali kwanza kabla ya mambo mengine (uwende kwa wazazi,(NDOA) pamoja na kwamba mahusiano yangu ya nyuma yalikuwa yana misuko suko mingi ila ww ni mwanaume ambae umemthamini Jacq,Nilipotoka niliteswa sn na mapnz yaani Usaliti,Dharau,kukosa mapnz ya dhati etc Pamoja ya kuwa pia alishatokea mmakonde na kunipeleka mpk mtwara na matembele nikachuma na wanakijiji kunipokea na kupikia familia na kutambulishwa kwa wazazi lkn sikufanikiwa kufikia hatua hii ambayo ww umefika!Umenijali na umenisikiliza nilipokwambia sihitaji mtu bali nahitaji future husband!Umekubali maamuzi yangu nilipokwambia km kweli unanipenda uende kwa wazazi nikijua ni mtego mkubwa nimekupa kumbe ww ndo kitu ulikua unakitaka kwangu😊Nashukuru sn Mungu kwa kunifunza kunyamaza ktk haya mahusiano kati ya mm na ww,Can't wait kesho moshi watakavyompokea mkwe wao kwa ajili ya mahari na kila kitu!(Ni mbege tu) Najiona mwenye bahati sn kumaliza mwaka kiaina hii na kuanza pia mwaka nikiwa na wewe….!Mungu akubariki kwa kuniamini na kuniona nitafaa nikiwa mkeo,Nyie dunia hii wakati wao waliniona sifai wakaenda kufata pesa,wanawake kuwatongoza na kuanza kunibadilikia lkn leo nimekupata ww ambae unaniuliza mbona walikuumiza sn na haukutakiwa kuumizwa,msemo wako mkubwa unaniambiaga nastahili kila kitu kizuri ktk hii dunia na sio maumivu…Nweiz staki kusema mengi lkn Namshukuru Mungu kwa kunipa wewe…!Sema wambea msijichoshe huyu sasa hayupo insta wala hajui haya mambo…! #AmSoExcited #HappyGirl #cantwaitformybigday 👌😍🙏

A post shared by Jacqueline Wolper (@wolperstylish) on

Hata hivyo kilichothibitisha kuwa Wolper ameachana na Brown(Ambaye yuko katika mitandao kwa jina la Brown) ni pale aliposema kuwa mpenzi wake wa sasa ambaye anaamini atabadilisha maisha yake ya kimahusiano kwa sailimia kubwa ni mtu ambaye ahayuko kabisa katika mitandao kitu ambacho kimekuwa kigumu kujua ni nani hasa.

Comments

comments

You may also like ...