Header

Rapa AKA na Bonang wapigana chini, AKA athibitisha

Rapa kutoka Afrika Kusini, AKA na mrembo mtangazaji maarufu, Bonang Matheba wameachana baada ya mahusiano yao ya kimapenzi kudumu kwa taribani miaka miwili sasa.

Himaker huyo ya ngoma ya ‘All Eyes On Me’ mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni mshindi wa tuzo kadhaa nchini humo alitangaza hilo la kuwa ameachana na Bonang kupitia mtandao wa twitter mapema jana asubuhi kwa kuandika “Myself and Bonang have decided to call it quits. I feel like I need to put this out there so we can both move on. I wish her all the best and I will always love her.”

Hii ndo tweet ya AKA

Awali kumekuwa na uvumi wa kuwa AKA na Bonang hawako vizuri baada ya kugundulika kuwa wameacha kuafuatana kwenye mitandao ya kijamii(Unfollow).Ambapo baadea AKA alikanusha kuwepo kwa hali ya kutoelewana kwa kusema ule ulikuwa ni uvumi tu ulisambaa kipindi cha mwezi Novemba mwaka huu.

Mapema mwaka huu, AKA pia alitangaza kuvunjika kwa mahusiano yake na Bonang lakini baadae aliweka sawa kuwa wamerijea kuwa pamoja na kutoa sababu kuwa ilikuwa ni katika hali ya kutokuelewana ambayo waliimaliza.

AKA na Bonang walianza kuwa na mahusiano mwaka 2015 na inadaiwa kuwa AKA ndiye sababu ya kuvunja kwa mahusoano yake ya kabla kati yake na mwanamke wake wa zamani ambaye pia ni mama wa mtoto wake ‘Kairo Owethu Forbes’, DJ Zinhle.

Comments

comments

You may also like ...