Header

Tiger Woods na matukio yake makubwa katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake

Ni katika kuikumbuka siku muhimu ya Mcheza Gofu maarufu Duniani, Tiger Woods ambaye kwa mwaka huu wa 2017 amekuatana na majanga ya kujikuta katika mikono ya sheria kwa makosa ambayo mastaa wengi ukumbana nayo.

Tofauti na hilo la kisheri, Tiger kwa mwaka huu aliingia latika habari njema ya wanaopenda anachokifanya kuwa atarejea uwanjani kuanzia Novemba 30 mpaka Desemba 3 baada ya kuwa akiugulia majeraha, taarifa ambazo ziliwakosha wengi waliokosa burudani yake ya umahiri katika mchezo huo.

Kisheria Tiger kwa mwaka huu mwezi Mei ameingia kwenye vichwa vya habari kwa tukio la kikamatwa katika mji wa Jupiter kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na baadae alikanusha kuwa hakuwa amelewa kwa msukumo wa pombe bali ni matumizi ya dawa ambazo alikuwa ameandikiwa na dakatari kuzitumia.

Katika tukio hilo lake ela kukamatwa, Tiger aliachiliwa huru kutoka gereza la Palm Beach County ambapo alikuwa nashikiliwa mida ya saa nne na nusu asubuhi.

Tarehe ya 30 mwezi Disemba ni kumbu kumbu ya kuzaliwa na mwanagofu huyu na leo anatimiza umri wa miaka 42, Kwa niaba ya Dizzim Online, anatakiwa heri ya maisha marefu na yenye mafanikio hasa katika ukanda wake wa kucheza mchezo huo ingawa anaoneana kuwa ni mwenye kukua zaidi kiumri.

 

Comments

comments

You may also like ...