Header

Kumbukumbu ya Kufariki kwa Muigizaji Sajuki

Katika kumbukumbu, Tarehe 2 Januari mwaka 2013 Muigizaji wa kiume kutoka katika tasnia ya Bongo Movie Tanzania, Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ alifariki Dunia kutokana na hali ya kuugua kwa muda mrefu ikiwa ni mwenye kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya ngozi, uvimbe tumboni na upungufu wa damu.

Hakika alikuwa ni kijana wa Kitanzania aliyekuwa na nia njema na tasnia hiyo ya filamu Tanzania na alikuwa ni mfano tosha wa kuigwa kwa kila vijana wa kileo wenye nia ya kujiajiri,kujikwamua na kupigana na vita dhidi ya adui umaskini.

Wapo ambao walisimama kwa utayari wa kumsaidia katika kipindi chote cha kuugua kwake kutoka ndani na nje ya tasnia akiwemo mke wake Wastara Juma.

Comments

comments

You may also like ...