Header

Man City kumkosa Jesus Pigo jingine ni De Bruyne, Silva na Stones

Vinara wa Ligi kuu nchini England Klabu ya Manchester City imethibitisha kumkosa Mshambuliaji wao Gabriel Jesus kufuatia majeraha ya Goti huku kukiwa na hati hati ya kuwakosa Kevin De Bruyne, David Silva pamoja na Jones Stones.

Jesus na De Bruyne waliumia katika Mchezo dhidi ya Crystal Palace ambao ulimalizika kwa Suluhu, taarifa kutoka kwa Madaktari wa Klabu hiyo imethibitisha kuwa Jesus atakua nje ya Mchezo huo ingawa jeraha lake la Goti si kubwa hivyo hatafanyiwa upasuaji, De Bruyne anaweza kucheza siku ya leo akitokea Benchi au akapumzishwa kabisa. Beki John Stones pamoja na kiungo David Silva wanaweza kurejea tena katika kikosi hicho baada ya kumaliza masuala yao binafsi.

Man City ambao hawajapoteza Mchezo wowote katika Ligi kuu wakiwa wamecheza jumla ya Michezo 20 watashuka tena Dimbani kwenye Mchezo wa Ligi dhidi ya Watford Mchezo utapigwa leo Januari 2 kwenye Uwanja wa Ethihad.

Comments

comments

You may also like ...