Header

AliKiba afungua mwaka na Cinderella baada ya kusindikizwa na Ommy Dimpoz

Staa AliKiba nchini Rwanda katika tamasha la East Africa Party la tarehe 1 mwezi Januari mwaka huu lililofanyika viwanja vya Amahoro vilivyoko mjini Kigali aliuchagua wimbo wa Cinderella uliobeba jina la Album yake ya mwaka 2007 kusafisha jukwaa katika kuufungua mwanzo wa Burudani.

Burudani hiyo iliyokuwa katika maadhi ya Reggae iliyopigwa live na kuwapagawisha zaidi mashabiki katika kuuanza mwaka na kingine kilichobainisha ni kuwa safari yake hiyo ya nchini Rwanda aliongozana na Mshikaji wake wa karibu Ommy Dimpoz.

AliKiba na Ommy Dimpoz

AliKiba kuwa pamoja na Ommy Dimpoz Nchini humo pengine ni ukaribu wao na ikizingatiwa kuwa ni mtu na Boss wake kwakuwa wawili hao wako chini ya mwavuli wa kampuni moja inayosimamia muziki wao ya RockStar4000.

AliKiba anahesabika katika ya mastaa walioingiza mtonyo kwa mfuatano wa matumuizo yailiyofanyika kwa mwishoni mwa mwaka 2017 na mwanzoni mwa mwaka wa 2018 ikiwa ni pamoja na hili ka kuufungua mwaka.

Comments

comments

You may also like ...