Header

Cardi B anaanza kuandika historia ya kimuziki Duniani

Mkali wa muziki wa Rap kutoka Marekani, Cardi B tangu ameachia wimbo wake kwa jina ‘Bodak Yellow’ uliofanya vizuri zaidi mwaka jana kwa kupata airplay kubwa sana, mambo yameanza kumuendea poa zaidi na kuoneakana kuwa ni muda wake sasa wa kuwaka kimuziki katika viwango vya juu.

Cardi B kila kazi ambayo ameshirikishwa kwa jina lake zinaonekana kupata nafasi nzuri sana hasa katika chati kubwa za muziki akiwa sasa hivi ameingia kwenye chati kubwa ya Top 100 za Billboard kwa kishindo.

Wiki hii Cardi B ameingiza ngoma tatu zenye jina lake katika orodha ya ngoma 10 Bora katika chati ya Billboard na kwa hilo amekuwa msanii wa tatu katika historia ya muziki kwa hatua hiyo ya kuingiza nyimbo zaidi ya moja kwa wachanaji(Marapa) wa kike.

Mafanikio ya nyimbo yake na alizoshirikishwa ambazo ziko katika orodha ya ngma zenye nafasi nzuri katika chati ya Billboard ni ngoma ya “No Limits” ya G-Eazy ambayo kwa sasa iko katika nafasi ya 4, Nyingine ni ngoma ya kundi la Migos ‘MotorSport,’ ambayo iko katika nafasi ya  7 na ngoma yake mwenyewe ya “Bodak Yellow iliyoko katika nafasi ya kumi.

Comments

comments

You may also like ...