Header

Davido auanza Mwaka 2018 na ‘ADA’

Staa wa Muziki kutoka nchini Nigeria David Adedeji Adeleke maarufu kwa jina la Davido amejipanga kuufungua Mwaka 2018 kwa kuachia ngoma Mpya siku ya Leo Januari 4 inayokwenda kwa jina la ‘ADA’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye Wafuasi zaidi ya Milioni Tano, Davido aliweka video fupi siku ya jana katika eneo la kumbukumbu la Matandao huo huku akiambatanisha ujumbe ulioandikwa “New Music Out tomorrow ADA” wenye maana ya Wimbo mpya unatoka kesho wenye jina la ADA.

Pia katika ukurasa wa Official Dj wa Davido ambaye ni DjeCool pia ameweka ujumbe unaoelezea ujio wa wimbo huo ambao umekamilika na utatoka leo hii huku akiandika kuwa Video na Audio zote zitatoka kwa wakati mmoja.

 

Hii inakua ngoma ya kwanza kwa Msanii Davido kutoa tangu Mwaka 2018 uanze lakini pia inakua ndio ya kwanza tangu nyota huyo amalize tofauti zake na Msanii mwenzake kutoka Nigeria Wizkid.

Comments

comments

You may also like ...