Header

Wolper aanza kuonekana na Engine baada ya tetesi za kutolewa mahari

Kijana ambaye amekuwa akisikika sana katika kufanya cover za nyimbo mbali mbali hasa za wasanii kutoka Tanzania, Sadiki Athanas’ anayefahamika zaidi kwa jina lake la sanaa ya muziki ‘Engine’ ameonekana katika picha tofauti tofauti akiwa na Jackline Wolper ndani ya vazi la mshono wenye kufanana na kutajwa kuwa ni mpenzi mpya wa Wolper.

Ibuka hii ya habari imekuja baada ya kuwa Wolper kusema kuwa amepata mpenzi mpya ambaye anajihisi kuletea firaha yenye kubeba maana halisi ya kupendwa hata kugusia kuwa mpenzi huyo mpya hapatikani mitandoni tetesi mpaka sasa zinabaki kuwa huu anayeanza kuonekana ndiye aliyesafiri mpaka nyumbani kwa familia ya Wolper kwa lengo la kukamilisha hatua za kumiliki jiko(Mke).

Kijana huyu ambaye wengi walikutana na sauti yake mara kadhaa kwa kurudia(Cover) nyimbo zilizopo katika orodha ya nyimbo zilizopata mapokezi mazuri na kufanya vizuri zaidi, alikitumia pia kipaji chake kuimba juu ya mada kubwa kubwa za kisanaa na zilizoonekana kuzungumziwa kwa ukubwa zaidi.

Engine alishaimba wimbo wa juu ya zile rusha rusha za madongo katika ya AliKiba, Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz ngoma kwa jina ‘Heshima Kwa Wanawake’ ambayo upo uwezekano wa kuwa ulishaisikia.

Comments

comments

You may also like ...