Header

Klopp ashikwa na kigugumizi Dili la Coutinho kwenda Barcelona

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameshindwa kuweka wazi kama tayari dili la kiungo wao Phillipe Coutinho kwenda Barcelona limekamilika kufuatia tetesi zinazoendelea katika Mitandao kuw akiungo huyo anaelekea Hispania katika dirisha Dogo la Usajili.

Jurgen Klopp amezungumzia suala hilo wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea Mchezo wao dhidi ya Everton katika kombe la FA unaopigwa Leo kwenye uwanja wa Anfield.

“Ninachoweza kusema kwa sasa zimekuwa zikiandikwa na kutungwa habari, mimi sina cha kuongea juu ya suala hilo, iko hivyo na hiki ni kipindi cha Dirisha dogo la Usajili ni hivyo tu sizani kama nina kingine cha kuongea” Alisema Klopp mbele ya Waandishi wa Habari.

Tangu dirisha kubwa la usajali la Mwezi Julai kufunguliwa klabu ya Barcelona imekuwa ikimuwania Mbazili huyo kwa hali na mali ambaye anatajwa ndiye mrithi wa Neymar ambaye alijiunga na PSG kwa rekodi ya Dunia.

Pia Kocha huyo amekiri kuwakosa Mohamed Salah pamoja na Philipe Countinho kwenye Mchezo dhidi ya Everton kutokana na Majeruhi ambayo watawafanya kukaa nje kwa muda wa Wiki moja huku kukiwa na uwezekano mdogo wa Mchezaji Sadio Mane ambaye alihidhulia sherehe za utowaji wa Tuzo za Mchezaji Bora wa Afrika nchini Ghana akiwa ni moja ya Washiriki lakini pia huenda Beki aliyesajiliwa kwa ada iliyoweka rekodi ya Dunia Virgil Van Dijik akacheza kwa mara ya kwanza kwenye Mchezo wa Leo.

 

Comments

comments

You may also like ...