Header

Nini na Nay wa Mitego wajibizana kimahaba

Rapa na muanzilishi wa lebo ya Free Nation kutoka Tanzania, Nay Wa Mitego ameufungua mwaka kwa ngoma ya mahaba aliyoshirikishwa na Mrembo Mwimbaji kutoka Tanzania ‘Nini’ ambaye walishasemekana kuwa wanatokana kimapenzi.

Ngoma hiyo inayokwenda kwa jina ‘Niwe Dawa’ iliyotayarishwa chni ya Studio za ‘Free Nation’ kwa mkono wa Producer Awesome, mrembo Nini anasikika akimbembeleza na kumhakikishia Nay kwa maneno ya  huba ambayo pia yanayoweza kuwatambulisha kama wapenzi.

“Ukitaka kulala, nami nilale twende ndotoni” Kwa Sauti inyoweza kumtoa nyoka Pangoni” Ni uandishi wa Nini anasikika akiimba.

Kisha Nay naye kwa sauti ya kiume iliyopondeka kwa maneno matamu inajibu juu ya hali zote zilizoelezwa na Nini ambapo kwa ufupi tu Nay anampa Sifa, Bila shaka ni sifa kwa nini kwa mstari unosema  “Napenda unavyoshika Mic, na unavyocontrol Show” ni uandishi wa Nay anasikika akichana.

Video ya ngoma hii imekuwa sana na muonekanao wa kupendeza na iliyosafi kwani kuna muonekano mmoja wa Nay ambao umewakilishwa na Suti matata ya rangi nyeupe ikiwa kazi nima imeongozwa na kuandaliwa na Director Deo Abel ambaye kwa wale wasio mfahamu zaidi ni kuwa ameshirikipia kuandaa na kuongoza video wa wimbo wa Prince Dully Sykes ‘Bombadier’.

Comments

comments

You may also like ...