Header

KIVURUGE YA NANDY INAVYOVURUGA MITAA KENYA!

Mwanadada na nguli wa vokali kali kwenye uga wa muziki kutoka hapa Tanzania almaarufu Nandy, huenda mwaka huu wa 2018 ukawa mwaka wake wa nema. Hii inatokana na kukubalika sana hadi na majirani nchini Kenya, naandika makala haya kutoka Mombasa Kenya na taarifa hii itakupatia twasira kamili kwa jinsi Nandy ameanza kujitengezea brandy Africa Mashariki na hata zaidi Africa. Katika ulimbwende wa sanaa na burudani ya muziki, nimekuwa mwepesi sana wa kutaka kusikiza jinsi mashabiki na wapenzi wa muziki wanavyosema kulingana na jinsi wasanii haswa wa Africa Mashariki wanavyotoa maoni kulingana na nyimbo kali zinazo shika chati na kusambaa ama (Ku-trend). Katika likizo yangu ya mwezi wa Disemba, ilinibidi niwe makini na kusoma ni msanii gani Africa Mashariki atakaye weza kuwapiku wenziwe kwa wimbo bora. Na hapa ndipo ngoma Kivuruge ya Nandy ilivyoweza kuingia kwa maskio yangu kila sehemu niliyofika.

Kwa mara ya kwanza nilisikilizishwa kivuruge na mdau na rafiki wangu wa karibu ambaye yeye huwa naamwamini sana hasa kwa jinsi anavyopenda kusikiliza muziki mzuri. Na baada ya hapo nikiwa kwenye likizo, nilitembea mjini Malindi na kila pahala nilipokanyaga sikusita kuusikia Kivuruge ikitema kwenye spika za maredio mjini Malindi. Kuanzia mtaa wa Ngala, Majengo, Kisumu Ndogo, Myeye na hadi vitongojini Nandy alikuwa anawika. Katika televisheni tofauti pia kubwa za nchini Kenya, Kivuruge tayari inaendelea kushika katika nafasi za juu kwa chati. Niliweza kuwahoji mashabiki na wendani wangu wa karibu kuhusiana na Nandy, na japo wengi walikuwa ndio kwanza wanamfahamu kupitia Kivuruge kunao walio fikiria sauti yake ni ya Ruby.

Nandy

Katika mkutadha huo, nikaamua basi kuchunguza zaidi mara tu niliporudi mjini Mombasa. Hali hapa Mombasa pia imekuwa ileile, ujumbe uliopo kwenye Kivuruge, vokali na hata video na mihemuko wa urembo wa kimwari huyu kwajina Nandy vimewachenua wengi na sikina dada,kaka,watoto pekee bali hadi watu wazima. Katika uchunguzi wangu wa kufatilia Kivuruge, nikaamua kuabiri gari kutoka mjini Mombasa hadi Ukunda sehemu ya pili ya Pwani Kusini. Kwenye matatu(Daladala) niliyopanda kuliwekwa mix ya Dj mmoja maarufu Kenya kwa jina Dj Bunduki. Katika mix hii mpya ya mwaka huu wa 2018, kivuruge ilichezwa zaidi ya mara moja. Katika bodaboda na kila sehemu ambapo nimepitia ikanibidi kuwa sina budi kukubali kwamba Kivuruge imekubalika zaidi. Nandy ananafasi nzuri sana kwasasa hapa Kenya, na uongozi wake unanafasi nzuri sana ya kuzichuna pesa kutoka kwa mashabiki wa muziki nchini Kenya ikiwa watachukua fursa hii ya Kivuruge kumukuza huyu mwanamuziki mkali kutoka Bongo.

Comments

comments

You may also like ...