Header

Chid Benz chini ya ulinzi kwa kosa la Madawa kwa Mara nyingine

Rapa na mkali wa mitindo huru, Rashid Abdallah Makwiro a.k.a Chid Benz kwa sasa taarifa zimeanza kusambaa kuwa yuko chini ya ulinzi baada ya usafiri waliokuwa wakiutumia yeye, Marafiki  zake na Mchumba wake kukutwa na kiasi cha madawa ya kulevya.

Chid Benz amejikuta katika msala huu mwingine wa madawa ya kulevya ambapo kamanda wa polisi Dodoma Gilles Muroto amethibitisha kuwa bado wote waliokamatwa na Chid Benz tangu tarehe 31 mwezi Disemba wanshikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

Chid Benz amekuwa katika matukio kadhaa ya kuhusishwa na madawa ya kulevya mara kwa mara kitu ambacho kimekuwa kikipokelewa tofauti na wadau na mashabiki katika hali ya utofauti huku wengi wao wakionesha kupoteza imani na Chid Benz.

 

Comments

comments

You may also like ...