Header

Bien wa Sauti Sol arusha kete za mistari kwa Tiwa Savage

Kolabo nyingine ya Nigeria na Kenya yaani kundi la muziki la Sauti Sol na mwimbaji Tiwa Savage imetoka ambapo imetoka sambamba na video ikiwa imeongozwa na Director Unlimited LA.

Bien-Aimé Baraza anasikika katika ubeti mmoja akijibizana kwa maneno yenye tafsiri ya huba na mrembo Tiwa Savage ambapo katika video sehemu ya wimbo huo ambayo wanabadilishana maneno katika video pia wanaoneshaka wakiimba wakitazmana na kuelekea kwa vitendo.

Ngoma hiyo inayokwenda kwa jina ‘Girl Next Door’ imekamilishwa na Supersonic Africa ambapo katika uandaaji pia maeshiriki mwimbaji ambaye pia ni mtayarishaji kutoka Nigeria, Maleek Berry.

Hata hivyo Sauti Sol wameahidi kuwa wanaachia kolabo waliyoshirikiana na wakali kutoka Afrika kila mwezi mapak mwezi Novemba mwaka huu.

ITAZAME VIDEO

Comments

comments

You may also like ...