Header

Diddy kutoa ofa ya $1m kwa dogo wa tangazo H&M kutangaza nguo za Sean Jean

Diddy ameripotiwa kumtafuta dogo aliyeonekana kwenye tangazo la kibaguzi la H&M ambalo limesababisha hasira kubwa duniani.

Picha hiyo inayomuonesha kijana huyo akiwa amevalia hood ya njano yenye maandishi ‘Coolest monkey in the jungle’ ilisambaa kwa kasi mtandaoni na kuwafanya mastaa kibao akiwemo Diddy walaani kitendo hicho cha ubaguzi wa rangi kilichofanywa na kampuni hiyo ya Sweden.

Na sasa Diddy anadaiwa kutaka kumpa mtoto huyo mkataba wa dola milioni 1 ili kutangaza nguo zake za Sean John, Metro.co.uk, imeripoti. Hata hivyo Diddy hajathibitisha tetesi hizo.

Kashfa hiyo imesababisha mastaa kama The Weeknd na G-Eazy kusitisha kufanya kazi na H&M ambayo imeomba radhi.

Comments

comments

You may also like ...