Header

Mimi Mars awapa sikio mashabiki juu ya nini kitoke kwa sasa

Mwimbaji kutoka Tanzania na Staa wa ngoma ya ‘Shuga’ Marianne Mdee ‘Mimi Mars’ amewapa sikio lake mashabiki juu ya nini kitangulie kati ya kuachia wimbo mpya na kuachia video ya wimbo wake uliotoka mwaka jana ‘Sitamani’.

Mimi ambaye alishaiambia Dizzim Online kuwa kwa ushirikiano na menejimenti yake wanajipanga kukamilisha video ya wimbo wake huo wa ‘Sitamani’ na jana alipost kupitia akaunti yake ya Snapchat kisha kushare ujumbe huo huo kwenye akaunti yake ya Instagram ambapo muda mfupi baada aliuondoa aliundoa kwenye ukurasa wake wa Instagram ujumbe ambao alikuwa akiwataka mashabiki wamwambie atangulize nini kwa sasa.

Mimi aliandika juu ya picha yake swali/ujumbe ulisomeka “Hivi niachie video ya Sitamani au nitoe tu wimbo mpya…” ujumbe uliowaacha mashabiki baadhi katika chaguo la kungoja video ya Sitamani kisha ifuate kazi mpya.

Comments

comments

You may also like ...