Header

Diamond Platnumz aonjesha sehemu jengo la ofisi mpya

Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ameonjesha video fupi ya baadhi ya maeneo ya jengo la ofisi mpya ya studio ya muziki ya WCB Wasafi na Studio zinazoashiria mpango wa kufugua kituo cha matangazo ya radio na Tv.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond alipost kipande kifupi cha video kinachoonesha jengo la kisasa, baadhi ya vifaa vya muziki na vifaa vya uendeshaji masuala ya matangazo ya redio na Tv na kuandika kuwa hilo ndo jengo jipya la makao makuu ya ofisi.

“NEW YEAR!! NEW HEADQUARTER!!!….Trust Me! You ain’t see Shit Yet…#WCB4Life” Aliandika Diaqmond Platnumz.

 

Hata hivyo Diamond Platnumz ameweka hilo wazi na kuonesha dalili za kuwa kinachofanyika kwa mwaka huu ni mabadiliko na kuonesha kuwa kipaji cha namna yoyote hasa katia upande wa sanaa kikitumika vilivyo upo uwezekano wa kufanya mambo makubwa kupitia mfano halisi wa anachokifanya yeye kupitia muziki.

Comments

comments

You may also like ...