Header

DOGO RICHIE: NAPANIA KUFANYA MAKUBWA 2018 KWENYE MUZIKI!

Dogo Richie kushoto akiwa na mtangazaji wa kituo cha Bahari FM cha nchini Kenya.

Akiongea na kituo cha radio cha Bahari FM kilichopo nchini Kenya, msanii na mkali wa kibao kinacho hit ”SAWA” maarufu kama Dogo Richie aliwaahidi mashabiki wake Africa mashariki kuwa watafurahi kwa jinsi alivyowapangia. Dog Richie ambaye kwasasa ndie msanii wa kutoka Pwani ya Kenya na mwenye maakazi yake mjini Mombasa anayefanya vizuri zaidi Africa Mashariki. Katika msimu huu wa likizo ya Disemba, staa huyu wa muziki kutoka Kenya alizuru hapa Tanzania mkoa wa Mwanza kwa shughuli za muziki. Tayari Richie ana kibao chake kipya alichokifanyia katika studio moja Mkoani Mwanza na amesema kibao hicho kitatoka baadaye wakati wake ukifika.

Akiongea na mtangazaji wa Bahari FM Pascal Shanga, alisisitiza kuwa heshima, uvumilivu na bidii yake kwenye muziki ndivyo vinamfunya kung’aa zaidi kuliko wasanii wengine. Habari kutoka nchini Kenya zina nadi kuwa huenda Dogo Richie akawa ndiye msanii wa Pwani ya Kenya aliyeingiza mtonyo mrefu zaidi kupitia show za muziki alizofanya kwenye mwezi Disemba pekee. Hadi sasa Dogo Richie yupo Jijini Nairobi akiwa katika harakati za media tour, akipania kujiuza zaidi kupitia media kubwa za nchini humo. Itakumbukwa kuwa wasanii wanaotoka Pwani ya Kenya huwa kila mara ndio wanaongoza katika muziki wa nchini Kenya hii ni kwasababu yakuwa niweledi na wanauzoefu wakuongea lugha ya Kiswahili sanifu. Hali ambayo inawapa msukumo wa kutunga mashairi mazuri na yakueleweka katika nyimbo hivyo mara nyingi hufananishwa na wasanii wakutoka hapa Bongo.

Comments

comments

You may also like ...