Header

MFAHAMU MPIGAJI PICHA STAA WAKITUO CHA RUNINGA YA NTV KENYE FESTO LANG.

Festo Lang akiwa na staa wamuziki kutoka Kenya Avril.

Je umeshawhi kukaa chini ukafikiria nikinanani waliopo nyuma ya pazia kwenye vyombo vya habari haswa runinga wanao husika na upigaji picha wakati vipindi vya runinga uvipendavyo vinaporushwa hewani? Je umeshawahi kukutana na mmoja wa wapigaji picha hawa? Kwa mara nyingi waongozaji wa vipindi, wapiga picha, wahariri na watu wengi wenye taaluma zao katika vyombo vya habari huwa sirahisi kujitokeza hadharani tofauti na wafanyavyo watangazaji maarufu wa habari na mastaa wengine wengi kwenye tasinia ya burudani ulimwenguni. Lakini leo kupitia meza yetu ya habari ya Dizzim, kalamu yangu imezama ndani hadi kwenye jumba la nation media group jijini Nairobi Kenya na ninakukutanisha na mmoja kati ya wapigaji picha stadi kwenye runinga maarufu inayotamba Africa iliyopo Kenya ya NTV.

Festo Lang kulia akiwa na mtangaza wa runinga ya NTV Kenya Larry Madowo.

Jina lake anaitwa Festo Lang ama unaweza muita Inuvu Jr. Yeye ni mmoja kati ya watu ambao walianzia chini katika tasnia hii ya upigaji picha. Huku kazi yake hii anasema alianzia kwenye viunga vya jiji la Nairobi, lakini bidii yake hii imemfanya mpka leo yupo nyuma ya camera kali na zenye nguvu duniani huku akiwa kupitia kazi yake hii ya upigaji picha ankutanishwa na watu maarufu si tu nchini Kenya bali dunia nzima. Mastaa wa hapa nchini Tanzania kama Diamond, Alikiba, Darassa ambao wameshawahi kuhojiwa na mtangazaji Larry Madowo wakati wa nyuma kwenye kipindi maarufu cha The Trend, ni baadhi ya watu maarufu ambao wameshawahi kupigwa picha na Festo kwani kwa wakati huu wote ameshakuwa nyuma ya kamera kwenye kipindi hiki cha The Trend wakati kilipokuwa kiki endeshwa na mtangazaji Larry Madowo kabla ya kuhamia kipindi chengine.

Festo Lang akihoji na mtangazaji wa habari maarufu wa runinga ya NTV Kenya kwajina Victoria Lubadiri.

Festo Lang anabidii ya mchwa na kutokana na kupenda kazi yake amefanikiwa kutembea duniani kwaajili ya kuchukua ama kupiga picha za habari tofauti kwaaajili ya kupeperusha hewani ili wapenzi na mashabiki wa runinga ya NTV nchini Kenya wanufaike na burudani. Hata hivyo hulka yake na kama wapiga picha wengine, Festo amekuwa mpole sana na sirahisi kujionyesha kwa umma. Mbali na kipindi cha burudani cha The Trend, Festo Lang pia hupiga picha kipindi maarufu cha NTV kwajina The Wicked Edition kinachoendeshwa na mcheshi maarufu wa nchini Kenya kwa jina Dr. King’ori. Kwa wale wanaofatilia runinga hii ya nchini Kenya ama kama umeshawahi kusafiri Kenya, unaweza kuwa unafahamu vyema kipindi hiki. Kipindi ambacho huleta watu maarufu wa nchini Kenya wakiwemo wanasiasa, wasanii wakubwa na kadhalika.

Comments

comments

You may also like ...