Header

Aslay aenda pekee yake kwa Snura

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mrembo mwenye majanga yake Snura Mushi ‘Snura’ ameitumia siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kwa kuachia kolabo yake na mkali wa Bongo Fleva Aslay inayokwenda kwa jina la ‘Moyo Nichae’.

Kolabo ya wimbo huo kutoka katika studio za Moja Moja Records umetoka siku hii maalumu kwa Snura ambapo mashabiki wa Aslay ni muda wao kumsindikiza Snura katika hii kubwa kwake ambapo wimbo huu umeandaliwa katika uandishi wenye kuzungumzia mahaba zaidi.

Snura mara hii anakutana tena na Aslay na kitu cha tofauti katika kolabo hii ni nje ya Yamoto Band kwakuwa walishakutana kipindi cha muunganiko wa kundi ambapo Snura alilishirikisha kundi katika wimbo wake uliokwenda kwa jina ‘Nionee Wivu’.

Comments

comments

You may also like ...