Header

Fid Q azidi kunenepa kwa ukaribu wake na mrembo huyu

Ili kuujua ukweli wa swali la kumtaja mrembo anayeusindikiza usingizi wa Rapa Fid Q katika maisha ya kuwajua wapenzi wa mastaa Tanzania sio rahisi kupata jibu sahihi na kila atakayeulizwa atatokewa na hali ya kigugumizi kwakuwa ukurasa huo wa maisha ya Fid Q hauko wazi kabisa.

Sio kawaida kwa Fid Q kuweka maisha yake binafsi katika macho na masikio ya wengi hasa kwa mashabiki wa muziki wake lakini kwa hili la kufuatana kwa picha zake na mrembo huyu ni ngumu kuamini kuwa wawili hao mipaka yao inaishia kwenye kingo za  urafiki tu.

Kama Fid Q atadai kuwa kumpost mara kwa mara mrembo huyu ni ugonjwa basi kwake huu umeshakuwa ugonjwa sugu kwakuwa dalili za rapa huyu msiri zinaonesha wazi kuwa kilichopo kati yake na mrembo huyu ni kikohozi ambacho tayari kukuficha inashindikana.

Hili limeibuka kwa sababu kila picha ambayo Fid Q uchukua maamuzi ya kuipost hasa kwenye ukurasa wake wa Instagram basi uambatana na maelezo sahihi na ya kueleweka ambayo mara kwa mara wengi wao ambao upata nafasi hiyo ya kutokea katika akaunti yake wanaambulia salamu za pongezi na kutakiwa maisha marefu katika siku za kumbukumbu za mfanano wa siku ya kuzaliwa kwao kitu ambacho ni tofauti kila ikipostiwa picha ambayo mrembo huyo atakuwepo.

Comments

comments

You may also like ...