Header

LavaLava amaliza video ya Kilio kwa masharti ya wazee

Msanii wa muziki kutoka Tanzania, LavaLava amesimulia majanga na mauza uza yaliyokwamisha baadhi ya vitu kutofanyika katika ukamilishaji wa video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina ‘Kilio’.

Wimbo huo uliotayarishwa chini ya Studio za WCB Wasafi huku video ikiongozwa na kampuni ya Zoom Production kutoka Tanzania chini ya Director Kenny, LavaLava amesimulia hali ya mauza uza iliyoibuka katika kijiji walikosafiri kwenda kufanikisha uchukuaji wa vipande vya video.

Akiongea na Dizzim Online, LavaLava amesema kuwa ulikuwa ni wakati mgumu sana kutokana na mambo mengi yenye ishara za ushirikina kuibuka hali iliyowalazimu kutafuta usaidizi na maelekezo ya nini kifanyike ili mambo yaende sawa.

Msikilize katika mahojiano na Dizzim Online.

Comments

comments

You may also like ...