Header

AY aongea kihispania kwa msisitizo juu ya upendo wa dhati kwa mpenzi wake

Staa wa muziki kutoka nchini Tanzania, Ambwene Allen Yessayah a.k.a AY ameweka bayana mipango yake ya siku za usoni juu ya kumuoa mpenzi wake ambaye amedumu naye katika mahusiano tangu mwaka 2008, mrembo anayetambuliwa na wengi kwa jina moja la Remy ambapo katika kuliwasilisha hilo  AY ametumia lugha nje ya lugha za Afrika Mashariki.

Kupitia ukurasa wa Instagram, AY aliweka ujumbe katika lugha ya Kihispania ambao kwa tafsiri ya kiingereza unasomeka “My beautiful future wife..Sweetheart..I love you so much” ambapo ujumbe huu haukuwa na habari mpya zaidi tu ulisisitiza kuwa kuna mategemeo ya kushuhudia ufungaji wa ndoa kati yake na  mrembo huyo.

AY mara hii ametumia lugha ya kihispania bila shaka kwa lengo la kuwafahamisha mashabibiki wa muziki wake na marafiki wote wenye uelewa wa lugha hilo katika msisitizo wa kuwa anampenda sana Remy na ndiye mwanamke wa maisha yake ya ndoa.

POST YA AY.

Comments

comments

You may also like ...