Header

Davido, Wizkid, Maleek Berry, Cassper Nyovest na wengine watamba usiku wa tuzo za SoundCity MVP 2018

STAA wa ngoma ya ‘IF’ kutoka nchini Nigeria, David Adedeji Adeleke a.k.a Davido ameibuka na ushindi mkubwa wa tuzo tatu za SoundCity MVP 2018.

Usiku wa tuzo hizo ziliofanyika mjini Lagos nchini Nigeria tarehe 12 Januari 2018, Davido aliweza kuimbuka kifua mbele kwa kushinda tuzo tatu kupitia kipengele cha Song of the Year kwa wimbo wake wa ‘IF’, Video of the Year(IF) na African Artist of the Year.

Mtayarishaji na muimbaji Maleek Berry alifuata kwa ushindi wa Tuzo mbili kupitia kipengele cha Best Pop na Best New Act huku Diamond Platnumz akiibuka na tuzo ya Best Male MVP, Wizkid alipata ushindi wa tuzo ya Digital Artist of the Year ambapo rapa  kutoka Afrika Kusini, Cassper Nyovest aliibuka na ushindi wa tuzo ya Best Hip Hop.

Hata hivyo Ushindi mwingine uliwaendea wakali wengine kama vile, Olamide, RunTown, Sarkodie, Tiwa Savage, Young Jonn na Distruction Boyz.

Comments

comments

You may also like ...