Header

Sappy ajiweka katika dalili za kuitamani kolabo na Sarkodie

Msanii na mtayarishaji wa muziki kutoka nchini Tanzania mwenye makazi yake nchini Kenya, Sappy ameonjesha mdundo na wazo la wimbo ambao imeonekana kama anapanga kumshirikisha mkali kutoka Ghana ‘Sarkodie’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sappy aliweka kipande kifupi video ukisikika mdondo na sauti zilizoimbwa na kuandika kuwa huo ni wimbo wake ambao mashabiki wanahitaji kuungoja na kilichoongezeka katika maelezo pale alipoongeza kwa maelezo mengine ambayo mwisho alimtag rapa Sarkodie.

Dizzim Online iliamua kumzamia Mtayarishaji huyo ili kujua ukweli hiki kinachoonekana kama ni ushirikiano ili kujua mipango iko vipi ambapo alionesha kutokuwa tayari kulizungumzia hilo kwa kina bali aliishia kwa kusema kuwa mwaka 2018 ni mwaka wa kutoka kwa baadhi ya kazi alizowatayrishia wasanii wakubwa na kuhusu Sarkodie akasema chochote kinaweza kutokea.

“Jamani waandishi msiwe na haraka kwasababu kazi ni nyingi sana, kila mmoja anataka kujua saaaana juu yangu na Sarkodie lakini nadhani kwa sasa ni mapema mno mimi kusema mengi, tusubirie tu. Kazi zipo na kwa mwaka huu yapo mengi ya kimataifa” Amesema Sappy.

Comments

comments

You may also like ...