Header

Jay Melody wa ‘Kivuruge’ ya Nandy aachia ‘Goroka’

Msanii mpya kabisa katika muziki wa Bongo Fleva kutoka Tanzania, Jay Melody ameachia rasmi video ya wimbo wake wa kwanza kutoka Epic Records ulioandaliwa na Producer Ringtone Beats ambapo video imeongozwa na Director DIDI.

Wimbo huo wenye uandishi wa bembelezo la mapenzi, Jay anautumia ufundi wa kumuelewesha mrembo asidanganyike na maisha ya hali ya juu na aridhike  na hali yao kwani kama ataridhia furaha itakuwepo kwakuwa anampenda sana mrembo huyo anayezungumziwa katika wimbo.

Walio wengi katika muziki wa Bongo Fleva hasa mwishoni mwa mwaka jana walianza kulisikia jina la Jay Melody baada ya kutoka kwa wimbo wa mwimbaji Nandy ‘Kivuruge’ kwakuwa katika taarifa za wimbo huo kusambaa na kusifiwa ilibainika kuwa Jay Melody ndiye aliyeandika na kuandaa wazo la wimbo huo.

Comments

comments

You may also like ...