Header

Simco akubali malalamiko yaliyo msukuma kuachia video ya ‘Come Over’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Simco hatimaye ameufungua mwaka wa 2018 katika muziki wake kwa video ya ngoma yake ‘Come Over’ ikiwa imeandaliwa na kupendezeshwa katika kioo cha watazamaji na Director Ivan.

Mtayarishaji aliyendaa audio ya wimbo huo sio mwingine bali ni Manster Madness na Simco ameimbia Dizzim Online kuwa ni furaha yake kuufungua mwaka na video wa wimbo wake huo kwakuwa alipata usumbufu mkubwa wa mashabiki kwa maswali ya ni lini video itatoka kwani wapo waliobahatika kuusikia wimbo mwaka jana.

“Huu wimbo umenishangaza kabisa, nilikuwa nikingoja muda niuachie rasmi lakini baadhi ya amshabiki walipata nafasi ya kuusikia na wakawa kila mara wananiulizia juu ya video jambo ambalo lilinifanya nisipoteze e kabisa, ikanibidi sasa niaachie kama hivi” Amesema Simco.

 

Comments

comments

You may also like ...