Header

Billnas alia na Ubunifu kwa Wasanii

Msanii wa hip hop nchini Billnass ametolea ufafanuzi juu ya jina la “MAFIOSO” baada ya mashabiki zake kutaka kufahamu hasa maana ya jina hilo ambalo amekuwa akiweka kwenye baadhi ya Post zake za kwenye ukurasa wa Instagram.

Akipiga story na DizzimOnline Rapper huyo amesema jina hiyo ni la kawaida tu na kama msanii si ajabu kuunda majina ya ajabu kwasababu kila siku msanii unatakiwa kuwa mbunifu

“Mafioso ni kama tu nickname  kwasababu huwa napenda hizo  yani kila siku nionekane mpya  na watu wanakubaatiza  kutokana na wanakuhitaji kila siku  so kila mtu ana namna yake anavyokuona so Mafioso ni member au mafia ndo wanakuwa Mafioso” alisema Billnass.

Aidha Billnass amewaomba mashabiki zake wakae mkao wa kula kwani muda si mrefu ataachia kazi yake Mpya na amewaambia kuwa haitakuwa na jina hilo la Mafioso.

Comments

comments

You may also like ...