Header

Hemed PHD afichua sura ya aliyempa heshima ya kuitwa Baba

Msanii wa maigizo na mwimbaji kutoka Tanzania, Hemed Suleiman ‘Hemed PHD’ tangu apate mtoto wa kiume aliyempatia jina la ‘Melody’ idadi kubwa ya mashabiki hasa wanomfatilia hawajapata bahati ya kuiona sura ya mrembo ambaye ndiye mama wa mtoto huyo wa kwanza wa Hemed.

Melody

Hemed ametoa fursa kwa mara hii kuiweka wazi wasioijua sura ya mama wa mtoto wake yaani Mama Melody. Kupitia ukurasa wa Instagram wa mtoto Melody ilipostiwa picha ya mrembo akiwa katika selfie na Hemed PHD na kuandika “Dear Mama…” ujumbe ambao moja kwa moja una maana ya kuwa huyu ndiye mrembo aliyepewa moyo na kuuchukua moyo wa Hemed PHD.

Mrembo aliyempa heshima ya kuitwa Baba Hemed PHD

Hata hivyo Melody anayejulikana kwa jina la VirgoChosen katika mtandao wa Instagram anacho kitu kikubwa cha kufanana na baba yake ambapo mbali kufanana sura, Melody amezaliza tarehe 30 Agosti (2016) tarehe ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Hemed Suleiman.

Comments

comments

You may also like ...