Header

Ruby akumbushwa na Babu Tale chakufanya asiyumbe kimuziki

Msanii wa muziki wa kizazi kipya mwenye sifa ya sauti nzuri na uandishi wa aina yake kutoka Tanzania, Ruby amekumbushwa juu ya kinachoweza kuwa ni sababu ya kulega lega kwake kimuziki mbali na kuwa ana uwezo mkubwa wa kuandika na kuimba.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mdau wa muziki, majasiriamali na meneja wa Staa wa muziki Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale ‘Babu Tale’, Ruby ameshauriwa kutumia muda wake kufanya utambuzi wake binafsi ili aweze kugundua na kurekesha kinachomuwekea kizingiti katika kuzipiga hatua za mafanikio ya kunufaika kwa ukubwa kupitia kipaji kikubwa alichobarikiwa.

Kikubwa kilichomsukuma Meneja Babu Tale kulisema hilo ni kutokana baadhi ya mambo yanayosemekana juu yake Ruby kushindwa kujua ni kwa namna gani anaweza kujiongezea thamani yake kama msanii kwani amegundua kuwa anaweza kufika mbali Zaidi kutokana na kile alichokiona kwenye kipande kifupi cha video anachomuonekana Ruby akiwa studio akiimba na kufatiliza uingizaji wa sauti Studio, kipande kinachopatikana katika tamthilia ya Kapuni.

Comments

comments

You may also like ...