Header

Paul Okoye wa P-Square apepea na nyingine ya peke yake ‘Nkenji Keke’

Msanii pacha aliyekuwa akiunda kundi la P-Square, Paul Okoye a.k.a RudeBoy amezidi kuweka jiwe baada ya jiwe kwa kuachia video ya ngoma yake ya mapenzi inayokwenda kwa jina ‘Nkenji Keke’, wimbo uliotayarishwa na producer Lord Sky na video kuongozwa na Director Mr. Moe Musa.

Video ya wimbo huo wa pili wa Paul, Director Mr. Moe Musa katika video hii alizingatia sana mavazi ya rangi nyeupe ambayo yanaonekana sana katika sare ya kufanana katika uvaaji wa Paul Okoye na mrembo aliyetumika katika video.

Ni miezi mitano sasa tangu kundi la mapacha la P-Square kujulikana wazi kuwa limevunjika ambapo Peter Okoye(Mr. P) na Paul Okoye(RudeBoy) mpaka sasa wanahesabika kuwa wameshaachia nyimbo mbili wakiwa ni wasanii wa kujitegemea nje ya kundi.

Comments

comments

You may also like ...